Maporomoko ya ardhi yasababisha maafa Murang’a

Tom Mathinji
1 Min Read
Mtu mmoja afariki kutokana na maporomoko ya ardhi kaunti ya Murang'a.

Mtu mmoja amefariki na mamia ya familia zikiachwa bila makao baada ya maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa katika kaunti ya Murang’a.

Kisa hicho kilitokea katika eneo la Ngutu, wakilishi wadi ya Gitugi, ambako takriban familia 200 zilipoteza makao, huku mipango ikitekelezwa ya kuwahamisha katika maeneo salama.

Maeneo mengine yaliyoathiriwa na maporomoko hayo ni pamoja na Karung’e, Kanjahi na Kahwai.

Wakati huo huo, familia kadhaa zimeachwa bila makao na mali kuharibiwa na maporomoko ya ardhi katika maeneo ya Gaikime, Kiagima Kiambuthia, Kagioini na Kora, kwenye wakilishi.

Maporomoko hayo ya ardhi  pia yamesababisha kuharibiwa kabisa kwa kanisa la Full Gospel Church Kamagogo.

Na katika wakilishi wadi ya Kamacharia, familia nne zimeachwa bila makao na mali ya thamani isiyojulikana kuharibiwa na maporomoko hayo ya ardhi.

TAGGED:
Share This Article