Kenya ilisherehekea siku ya kimataifa ya riadha ya wototo ambayo huadhimishwa kila mwaka Mei 7,kwa kuandaa mashindano baina ya watoto wa shule kote nchini.
Katika kaunti ya Nairobi zaidi ya watoto 300 kutoka shule kadhaa walikongamana katika shule ya msingi ya Toi, mtaani Kibera, kushindana katika michezo mbalimbali.
Kaunti za Kericho ,Baringo na Mumias, pia ziliandaa mashindano sawia na hayo baina ya wanfunzi .
Lengo la siku hiyo ni kuwapa watoto fursa ya kudhihirisha vipaji vyao huku wakufunzi wakihitajika kuwa na ubunifu wa hali ya juu katika kuwashirikisha wanafunzi katika fani mbalimbali za michezo.
Mashindano hayo baina ya watoto yataendelea hadi Mei 30, huku kila taifa likihitajika kuwasilisha picha za maadhimisho ya siku hiyo huku mshindi akituzwa dola 10,000.
Kenya ilitawazwa mshindi mwaka jana na kutuzwa shilingi milioi 1.2 .
Kaulimbiu ya mwaka huu ni kusherehekea miaka mitano tangu kuanzishwa kwa riadha ya watoto.