Waziri wa Afya nchini Kenya Aden Duale siku ya Jumatatu amezindua Baraza jipya la matabibu na wataalam wa meno nchini (KMPDC) , itakayoongozwa na Profesa Namenya Were.
Akizungumza baada ya kuzindua baraza hilo Duale, ametaja wajibu muhimu unaotekelezwa na wataalam hao katika afya ya jamii na kusisitiza haja ya kuzingatia kanuni za kitaaluma.
Waziri pia alitaja mabadiliko yanayoendelea katika sekta hiyo yatakayopiga jeki juhudi za serikali za kutoa huduma bora za matibabu kwa wananchi.
Alilitaka baraza hilo kuwa katika mstari wa mbele kuleta mabadiliko mwafaka ya kuleta uwazi na usimamizi bora.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Katibu wa Afya ya umma Mary Muthoni,Mkurugenzi mkuu wa Afya Dkt Patrick Amoth,na Afisa Mkuu mtendaji wa KMPDC David Kariuki miongoni mwa viongozi wengine wa wizara ya afya.