FIFA World Cup: Uhispania yawatema nje majirani Ureno

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa wa mwaka 2010 Uhispania walikuwa na wakati mgumu kabla ya kuwatema nje majirani Ureno katika mechi ya raundi ya 16 ya Kombe la Dunia Jumatatu usiku.

Mechi ikielekea kumalizikia sare tasa katika uwanja wa Dallas, nguvu mpya Mikel Merino alipata pasi murua na kutumbukiza mpira langoni kunako dakaka ya 91.

Ni mara ya kwanza kwa Uhispania kufika robo fainali tangu mwaka 2010 walipotwaa kombe hilo nchini Afrika Kusini.

Uhispania watakabiliana na Ubelgiji katika robo fainali.

Share This Article