Rais Ruto: Lengo letu ni kuliunganisha taifa hili

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto akiwahutubia viongozi wa kaunti za Kisii na Nyamira katika Ikulu ndogo ya Kisii.

Rais William Ruto amesema lengo kuu la serikali yake ni kuliunganisha taifa kupitia mpango wa kuimarisha uchumi wa Bottop Up na kufanikisha ukuaji katika maeneo yote ya taifa.

Kiongozi wa taifa alisema wanajizatiti kuimarisha serikali jumuishi kupitia mashauriano ya mara kwa mara na viongozi wa mashinani na wale waliochaguliwa.

“Hatua hii hutuleta karibu na maswla yanayowakabili wakenya, na kuhakikisha hatua tunazochukua zimebuniwa na watu wetu,” alisema Rais Ruto.

Rais Ruto aliyasema hayo siku ya Jumatatu alipokuwa mwenyeji wa viongozi zaidi ya 2,000 kutoka kaunti za Kisii na Nyamira katika Ikulu ndogo ya Kisii.

Kwenye mkutano huo, Rais na viongozi hao walikubaliana kuharakisha utekelezwaji wa miradi ya maendeleo huku taifa hili likijitahidi kuwa nchi iliyostawi duniani.

Awali Rais alikagua ujenzi unaoendelea wa soko la kisasa la Nyakoe lililoko eneo bunge la Kitutu Chache Kusini, kaunti ya Kisii.

Litakapokamilika, litawahifadhi wafanyabiashara 300.

Share This Article