Maafisa kutoka asasi mbalimbali za usalama, wamepta mifugo 101 waliokuwa wameibwa katika kaunti ya Laikipia.
Operesheni hiyo ilitekelezwa katika maeneo ya Arjijo, Anandangu’ro, na Lokosero ambayo awali yalitajwa kuwa hatari kwa ujangili na wizi wa mifugo.
Kupitia ukurasa wa X, Huduma ya Taifa ya Polisi, ilisema mifugo hao waliopatikana walipelekwa katika kituo cha polisi ambako wanasubiri kutambuliwa na kukabidhiwa wenyewe halisi.
“Kupatikana kwa mifugo hao kunaashiria hatua muhimu katika kukabiliana na visa vya uhalifu na kusambaratisha mitandao ya wahalifu katika eneo hilo kupitia operesheni za asasi mbali mbali na ushirikiano na jamii,” ilisema Huduma hiyo ya Polisi.
Huduma hiyo ilisema imejitolea kukabiliana na wahalifu na kuhakikisha jamii zilizoathiriwa zinalindwa.