Serikali ya Israeli inafanya mipango ya ujenzi wa nyumba 5,700 mpya katika ukingo wa magharibi ya mto Jordan.
Tangazo hilo limewadia licha ya Marekani kushinikiza kusimamishwa kwa upanuzi wa makao ambao inaonelea kuwa kizingiti kwa shughuli ya kutafuta amani na wapalestina.
Kulingana na hatibu mmoja wa Marekani, nchi hiyo imekerwa na mpango huo.Masetla wanne wa Israeli waliuawa kwa kupigwa risasi na wapalestina wiki iliyopita na kuibua ghasia.
Ghasia kati ya Wapalestina na Israeli zimeongezeka tangu waziri mkuu Benjamin Netanyahu achaguliwe tena mwaka uliopita.
Serikali yake imesema itapanua makao katika ukingo wa magharibi ya mto Jordan.
Kulingna na kundi linalopinga ujenzi wa makao hayo la Peace Now, zaidi ya nyumba 13,000 mpya zimejengwa katika ukingo wa magharibi ya mto Jordan.