Natembeya achunguzwa na EACC, kwa kulipa kiholela zabuni ya shilingi bilioni 1.4

Natembeya anachunguzwa kwa madai ya kukiuka sheria za utoaji zabuni nchini alipotoa kandarasi tatu tofauti.

Dismas Otuke
1 Min Read

Gavana wa Kaunti ya Trans Nzoia, George Natembeya, aemefikishwa katika makao makuu ya tume ya maadili na kupambana na rushwa nchini (EACC), Jumatatu jioni kujibu mashtaka ya matumizi mabaya ya afisi.

Maafisa wa EACC, wamefanya msako nyumbani kwa Gavana huyo mapema Jumatatu, kuhusiana na zabuni alizotoa za shilingi bilioni 1.4, katika kipindi cha matumizi ya fedha cha mwaka 2022-2023 na 2024 na 2025.

Natembeya anachunguzwa kwa madai ya kukiuka sheria za utoaji zabuni nchini alipotoa kandarasi ya ukarabati wa uwanja wa Kenyatta mjini Kitale, ujenzi wa makao makuu ya kaunti hiyo na ujenzi wa hospitali ya Tom Mboya.

EACC inadai kuwa Natembeya, alihusika katika kushawishi utoaji wa zabuni, na kisha akapokea mrungula akishirikiana na Mhasibu Mkuu wa kaunti Emmanuel Masungo, msimamizi mkuu wa maji Dorothy Nyukuri, Mkurugenzi wa zabuni Eliyah Liambula na Desmond Shivachi, ambaye anaaminika kuwa Mkandarasi gushi wa Gavana Natembeya.

Website |  + posts
Share This Article