Ziara ya Rais Ruto Mlima Kenya yaingia siku ya pili

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais Ruto azindua miradi ya maendeleo eneo la Mlima Kenya.

Ziara ya Rais William Ruto katika eneo la Mlima Keny  inaingia siku ya pili leo Jumatano huku akitarajiwa kuzindua na kukagua miradi ya maendeleo katika kaunti za Meru na Kirinyaga.

Rais Ruto anatarajiwa katika maeneo bunge ya Igembe Kusini, Tigania Magharibi, Imenti Kusini, Mwea na Kirinyaga.

Kiongozi wa taifa alisema ziara hiyo ya Mlima Kenya inalenga kuwafahamisha wananchi kuhusu miradi inayotekelezwa na serikali yake.

Ameahidi kufanya kazi na Wakenya wote kwa lengo la kuunganisha taifa na kuboresha hali ya maisha.

Rais Ruto alisema, ili maendeleo yapatikane humu nchini, Wakenya wanapaswa kukomesha siasa za chuki na ukabila.

Jana Jumanne, kiongozi wa nchi alizuru kaunti za Laikipia na Nyeri, alikozindua mradi wa usambazaji umeme  wa Last Mile Connectivity na kufungua rasmi nyumba 200 za gharama nafuu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *