Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliiambia Fox News siku ya Jumanne kwamba Ukraine itapoteza vita ikiwa Marekani ambayo ni mfadhili wake mkuu wa kijeshi, ataondoa ufadhili.
Kiongozi huyo wa Ukraine amesema itakuwa “hatari sana iwapo tutapoteza umoja barani Ulaya, na lililo muhimu zaidi ni umoja kati ya Ukraine na Marekani”.
Rais mteule wa Marekani Donald Trump amefanya kampeni kwa ahadi ya kukomesha ushiriki wa Marekani katika vita na badala yake kutumia pesa za walipa kodi kuboresha maisha ya Wamarekani.
Amesema atamaliza vita vya Urusi na Ukraine ndani ya saa 24, bila kusema kwa namna gani.
“Ikiwa watakata, nadhani tutapoteza,” Zelensky aliiambia Fox News.