Waziri wa Utumishi wa Umma Geofrey Ruku ametangaza azma ya kuwania kiti cha Ugavana wa gatuzi la Nairobi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Amesema atagombea kiti hicho kwa tiketi yua chama cha United Democratic Alliance (UDA).
Ruku ameahidi kurekebisha makosa yaliyofanywa na Gavana wa sasa Johnson Sakaja, akihoji ni kwa nini wakazi wa Nairobi wangali wanalalamikia changamoto za muda mrefu za huduma duni.
Waziri alisema wakazi wa kaunti ya Nairobi wanahitaji huduma bora kama vile njia mwafaka za uzoaji taka na kumaliza uhaba wa maji wa mara kwa mara.
Ruku anajiunga na msafara wa wanaomezea mate kiti cha Ugavana wa Nairobi.
Wao ni pamoja na wabunge Babu Owino wa Embakasi Mashariki (Linda Mwananchi), James Gakuya wa Embakasi Kaskazini (DCP), George Aladwa wa Makadara (ODM), na Ronald Karauri wa eneo bunge la Kasarani.
Aidha, aliyekuwa msimamizi mkuu wa kaunti ya Nairobi Geoffrey Mosiria na Askofu Margaret Wanjiru pia wanamezea mate wadhifa huo.
Wagombea wengine ni Katibu wa zamani Irungu Nyakera na mfanyabiashara Agnes Gakure huku wakikabiliana na Sakaja ambaye ametangaza kutetea kiti chake kwa tiketi chama cha ODM baada ya kugura UDA.