Seneta mteule Veronica Maina ameteuliwa kuwa naibu wa walio wengi katika bunge la Seneti.
Wadhifa huo awali ulishikiliwa na Seneta Tabitha Karanja, aliyeenguliwa baada ya kugura chama cha UDA na kujiunga na DCP.
Maina aliinjikwa kumrithi Seneta Karanja Novemba 3 kupitia uamuzi wa Maseneta wa UDA na kisha kiranja wa wengi katika bunge la Seneti kuwasilisha mabadiliko hayo kwa Spika Amason Kingi.
Kingi alitangaza na kuthibitisha mabadiliko hayo siku moja baadaye.
Karanja alichaguliwa Seneta wa Nakuru kwa mara ya kwanza mwaka 2022 kupitia UDA.
Maina atakuwa naibu wa walio wengi katika Seneti akimsaidia Seneta Aaron Cheruiyot katika majukumu ya kuwasilisha na kutetea miswada ya serikali katika bunge hilo.