Mama akamatwa kwa kumkeketa mwanawe Dandora

Mtoto huyo ambaye tayari alikuwa amekeketwa, alipelekwa katika kituo cha Afya cha Dandora Phase 3, ambako alipokea matibabu na kuruhusiwa kuondoka hospitalini.

Tom Mathinji
1 Min Read
Mwanamke akamatwa kwa kumkeketa mwanawe Dandora.

Maafisa wa Polisi wamemkamata mwanamke wa umri wa miaka 32, kwa madai ya kumkeketa mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 8.

Frolence Ngendo Nyambura, alikamatwa na maafisa wa polisi walioandamana na afisa wa watoto wa kaunti hiyo ndogo baada ya majirani kumfumania akitekeleza uovu huo katika mtaa wa Dandora Phase 2.

Mtoto huyo ambaye tayari alikuwa amekeketwa, alipelekwa katika kituo cha Afya cha Dandora Phase 3, ambako alipokea matibabu na kuruhusiwa kuondoka hospitalini na kupelekwa sehemu salama kufanikisha ulinzi wake.

“Mshukiwa huyo anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Dandora,akisubiri kufunguliwa mashtaka ya kushiriki ukeketaji kinyume na sehemu ya 19(1)  ya sheria za FGM  2011, miongoni mwa mashtaka mengine,” ilisema Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI), kupitia ukurasa wa X.

Huduma ya Taifa ya Polisi ilisema itajizatiti kukabiliana na uovu huo na kulinda haki ya kila mtoto kukua kwenye mazingira safi na yasio na aina yoyote ya ghasia.

TAGGED:
Share This Article