Mama Taifa Rachel Ruto, amewasili katika Ufalme wa Morocco kwa ziara rasmi ya kikazi, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa pande mbili na kuimarisha utoaji huduma za afya.
Alipowasili nchini Morocco akiwa ameandama na katibu wa huduma za matibabu Dkt. Ouma Oluga, Mama Taifa alilakiwa na mstahiki Sultana wa Morocco Lalla Asmaa.
Kupitia ukurasa wa X, Mama Taifa alisema ziara hiyo inatarajiwa kuimarisha uhusiano wa Kenya na Morocco na juhudi za pamoja za kuimarisha ujumuishaji, hadhi na fursa sawa kwa watoto walio na ulemavu wa kusikia.
“Ninatazamia kwa majadiliano yanayolenga kuleta fursa na matumaini kwa watoto walio na ulemavu wa kusikia,” alisema Mama Taifa.
Kupitia ushirikiano huo, wataalam wa matibabu kutoka hospitali ya kitaifa ya chuo kikuu ya Mafunzo, utafiti na Rufaa cha Kenyatta, ile ya chuo kikuu cha mafunzo na rufaa cha Moi na hospitali ya MP Shah, wamepokea mafunzo ya kitaalam ya upasuaji wa masikio na matibabu mengine ya masikio, na hivyo kuimarisha uwezo wa Kenya wa kutoa huduma zilizoimarika za matibabu ya masikio.