Waziri Owalo asaini mkataba na UNDP

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali ya Kenya kupitia kwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Kidijitali, imesaini mkataba wa maelewano na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, UNDP.

Waziri Eliud Owalo amesema wako katika mchakato wa kuboresha uhusiano na kupanua mipaka ya kibiashara na upatikanaji wa huduma zote za serikali kupitia mtandaoni.

“Tutafanya kazi na shirika la UNDP kukuza ueneaji wa mifumo ya kidijitali nchini Kenya. Katika mchakato huo, tutakuza kazi za mitandaoni kuhakikisha huduma zinapatikana kwa bei nafuu kwa watu wengi, ”alisema Waziri Owalo.

Hafla hiyo ya mapema leo Jumatatu, ilihudhuriwa na makatibu katika wizara hiyo Mhandisi John Tanui, Profesa Edward Kisiang’ani, Amos Kateshe wa Wizara ya Utumishi wa Umma na maafisa wengine wakuu serikalini pamoja na Ahunna Eziakonua ambaye ni mkurugenzi wa ukanda wa Afrika wa shirika la UNDP.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *