Waziri Ogamba awaonya wanaosambaza mitihani bandia

Kanyali Boniface
1 Min Read
Waziri Julius Ogamba (kulia) alipozuru kaunti ya Kitui

Waziri wa Elimu Julius Ogamba ametoa onyo kali kwa wanaosambaza mitihani bandia kwa kisingizo kuwa ni ya Baraza la Mitihani nchini, KNEC, akisema watachukuliwa hatua kali za kisheria. 

Ogamba amewahakikishia Wakenya kuwa matayarisho kabambe yamefanywa kuhakikisha mitihani ya kuandikwa ya KNEC inaanza vyema Novemba 3, 2025.

Aliyasema hayo aliposhuhudia ufunguzi wa kontena ya mtihani wa tathmini wa KNEC katika ofisi ya kamishna wa kaunti ya Kitui.

Waziri akitumia fursa hiyo kusisitiza kuwa wizara yake kwa ushirikiano na Wizara ya Usalama wa Taifa imeimarisha usalama kuhakikisha usimamizi mzuri wa mitihani hiyo.

Pia alisema anafahamu mipango ya wahalifu kutilia doa uadilifu wa mtihani hiyo kwa kusambaza mitihani bandia mtandaoni na kuonya kuwa wahusuka watachukuliwa hatua kali za kisheria.

 

Kanyali Boniface
+ posts
Share This Article