Wakenya waombwa kukumbatia mazungumzo, njia mbadala za kusuluhisha mizozo

Martin Mwanje & Carolyn Necheza
1 Min Read
Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Renson Ingonga (katikati, mstari wa mbele) wakati wa kongamano mjini Kakamega

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Renson Ingonga ametoa wito kwa Wakenya kukumbatia mazungumzo na njia mbadala za kusuluhisha mizozo badala ya kukimbilia mahakamani kila wanapozozana.

Akizungumza wakati wa kongamano la uhamasishaji wa umma mjini Kakamega, Ingonga alisema usuluhishaji mizozo kwa njia ya amani husaidia kutunza urafiki na kupunguza mrundiko wa kesi.

Aliongeza kuwa wananchi wengi hawaelewi kikamilifu namna mfumo wa sheria unavyofanya kazi chini ya katiba ya mwaka 2010.

DPP akitoa wito kwa umma kutafuta ushauri wa maafisa wa sheria kabla ya kuchukua hatua.

Kulingana naye, ukosefu wa uelewa mara nyingi huwafanya watu kuelekea kwenye taasisi zisizostahili wanapozozana.

Kongamano hilo liliwaleta pamoja na washikadau wakuu kutoka mfumo wa sheria na wananchi ili kujadili upatikanaji wa haki na kuboresha ushirikiano miongoni mwa wadau katika sekta ya haki.

Nalo liliratibiwa na Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma na Misheni ya Kimataifa ya Haki, IJM.

Martin Mwanje & Carolyn Necheza
+ posts
Share This Article