Watu wawili wametiwa mbaroni na polisi kuhusiana na kaburi la pamoja lililopatikana katika kaunti ya Kericho jana Jumapili.
Waliokamatwa ni Afisa wa Afya ya Umma katika kaunti ya Nyamira David Araka, na mlinzi wa makaburi hayo Richard Towett.
Hii inafuatia kupatikana kwa mili 14 iliyokuwa imezikwa ndani ya kaburi moja katika eneo la Makaburini.
Hata hivyo, kesi dhidi ya washukiwa hao huenda ikachukua muda mrefu kabla ya kuanza kusikizw baada ya polisi kuiomba mahakama kuwapa siku 30 zaidi ili kukamilisha uchunguzi.
Ukweli unatarajiwa kubainika baada ya korti kutoa kibali kwa polisi kufukua kaburi hilo na miili hiyo kufanyiwa uchunguzi wa DNA na Patholojia mkuu wa serikali.
Maafisa wa kaunti ya Nyamira walikiri kusafirisha mili 13 Alhamisi iliyopita hadi kwenye makaburi hayo yanayoaminika kumilikiwa na Baraza la Makanisa nchini (NCCK) kutokana na ukosefu wa maziara katika kaunti hiyo.
Maziara hiyo imewekwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.