Watu kadhaa wafariki kwenye ajali ya barabarani Makueni

Waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo walipelekwa katika vituo vya afya vilivyo karibu kwa matibabu.

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu kadhaa wafariki kwenye ajali ya barabarani katika eneo la Salama, kaunti ya Makueni.

Watu kadhaa wameaga dunia, baada ya kuhusika kwenye ajali ya barabarani katika eneo la Salama, kaunti ya Makueni.

Ajali hiyo iliyotokea kwenye Barabara Kuu ya Nairobi – Mombasa Jumamosi asubuhi, imehusisha gari la abiria 14 na lori la kubeba mizigo.

Waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo walipelekwa katika vituo vya afya vilivyo karibu kwa matibabu.

Duru zinasema kuwa ajali hiyo ilisababishwa na lori hilo ambalo lilipoteza mwelekeo baada ya kupata hitilafu za breki na kugonga magaro kadhaa, ikiwemo matatu hiyo ya abiria 14.

Eneo hilo la Salama limenakili ajali kadhaa hapo awali, na ambazo zimesababisha maafa na majeraha kwa wasafirii, ya hivi punde ikiwa ile iliyotokea Juni 8, iliyohusisha magari manne.

TAGGED:
Share This Article