KUCCPS yakaa ngumu, yadinda kutoa orodha ya wanafunzi wa kuingia vyuoni

KUCCPS imesema itatoa tu orodha hiyo kwa vyuo vilivyowalisha pesa zinazohitajika au kutoa mpango wa kulipa madeni hayo.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mamlaka ya kuwateua wanafunzi wa kujiunga na vyuo vikuu na vile vya kiufundi nchini Kenya (KUCCPS), imesimama kidete na kudinda kutoa orodha ya wanafunzi walioteuliwa kujiunga na vyuo mbalimbali kwa vyuo vilivyo na malimbikizi ya madeni.

KUCCPS imesema itatoa tu orodha hiyo kwa vyuo vilivyowalisha pesa zinazohitajika au kutoa mpango wa kulipa madeni hayo.

Kwa kawaida, vyuo hutoza kila mwanafunzi ada ya shilingi 1,500 ya usajili inayolipwa wakati mwanafunzi anapoingia chuoni ambayo inapaswa kuwasilishwa kwa KUCCPS.

Hata hivyo, KUCCPS inadai jumla ya deni la shilingi nusu bilioni kutoka kwa vyuo vikuu na vile vya kiufundi.

TAGGED:
Share This Article