Mamia ya raia wa Burundi walimiminika katika ubalozi wa Nairobi kwa siku ya tatu mfululizo kujisajili ili kupata stakabadhi za kuishi na kufanya biashara nchini Kenya.
Hii ni baada ya serikali kutoa makataa ya siku 90 kwa raia wote wa kigeni wanaoishi Kenya kujisajili la sivyo watimuliwe.
Foleni ndefu zilishuhudiwa kwenye Ubalozi wa Burundi katikakati ya jiji kwa shughuli hiyo.
Kenya ina jumla ya wakimbizi 16,000 raia wa Burundi wanaotafuta hifadhi ya ukimbizi huku idadi hiyo ikizidi kuongezeka kutokana na misukosuko ya kisiasa ambayo imekuwa ikishuhudiwa nchini mwao.
Wengi wa waliofika katika ubalozi wanaelezea kuhofia maisha kufuatia agizo la Rais William Ruto wiki jana, baadhi wakikiri kuhangaishwa na Wakenya.