Timu ya taifa ya Kenya kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 23 ,Emerging Stars imeondoka nchini mapema Jumamosi kuelekea Dar es Salaam kwa mechi ya ,marudio raundi ya kwanza kufuzu kwa fainali za kombe la AFCON mwaka ujao.
Kenya ilikamilisha mazoezi yake jana kujiandaa kwa mchuano huo huku wachezaji waliostaafu wakiwapa wachezaji hao mawaidha.
Kenya inayoongoza mabao 4-1 kutokana na duru ya kwanza itakumbana na wenyeji Jumanne Oktoba 6 huku ,mshindi akifuzu kwa raundi ya pili kukabiliana na Ivory Coast .
Timu saba pamoja na wenyeji Misri zitafuzu kwa fainali za AFCON mwaka ujao ambazo pia zitatumika kufuzu kwa michezo ya Olimpiki ya mwaka 2028.