Shirikisho la kandanda barani Afrika (CAF) limehiari kurejelea fainali za mashindano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika kila baada ya miaka miwili.
Kamati kuu ya CAF ilikutana na kuafikiana kubadilisha uamuzi wa awali wa kuandaa fainali za AFCON, kila baada ya miaka minne.
Fainali zijazo za 36 zitaandaliwa mwaka ujao kwa pamoja na mataifa ya Kenya,Uganda na Tanzania.
AFCON ya 37 itafanyika mwaka 2028,ikifuatwa na ile ya mwaka 2031 na kisha 2033