Watu 13 wafariki kwenye moto katika eneo la burudani Uhispania

Marion Bosire
1 Min Read

Watu wapatao 13 walifariki kwenye mkasa wa moto uliotokea jana Jumapili alfajiri katika eneo moja la burudani nchini Uhispania.

Moto huo ulizuka katika kilabu hicho cha usiku cha orofa mbili kiitwacho “Teatre” au “Fonda Milagros” katika mji wa Murcia uliopo eneo la Kusini Mashariki la Uhispania.

Meya wa mji wa Murcia Jose Ballesta alisema moto huo ulizuka saa 12 asubuhi saa za nchi hiyo na ulikuwa mkubwa sana.

Wahudumu wa kuzima moto walifika eneo la mkasa saa moja asubuhi saa za Uhispania na wakafanikiwa kuuzima kufikia saa mbili asubuhi.

Maafisa wa usalama walisema watu wanne walijeruhiwa kwenye kisa hicho na wanatibiwa kutokana na madhara ya moshi.

Inaripotiwa kwamba moto huo ulianzia kwenye sehemu ya chini ya kilabu hicho na kisha kusambaa hadi orofa ya kwanza, lakini chanzo hakikubainika mara moja.

Share This Article