Abraham Kithure Kindiki ambaye ataapishwa kuwa Naibu Rais leo Ijumaa katika ukumbi wa KICC, alizaliwa Julai 17 mwaka 1972 katika wilaya ya Meru.
Kindiki alisomea shule ya Lenana na baadaye ile ya Tharaka Boys High School na alipata shahada ya uanasheria kutoka Chuo Kikuu cha Moi mwaka 1998.
Miaka miwili baadaye Kindiki alipata shahada ya uzamili ya uanasheria kutoka Chuo Kikuu cha Pretoria nchini Afrika Kusini.
Pia alipata stashahada ya uanasheria kutoka kutoka chuo cha sheria nchini mwaka 2001 na baadaye akapata shahada ya uzamifu ya uanasheria kutoka chuo cha Pretoria nchini Afrika Kusini mwaka 2002.
Katika kuchapa kazi, Kindiki alikuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Moi mwaka 1999, kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Nairobi mwaka 2024 na kurejea tena katika Chuo Kikuu cha Moi mwaka 2005 kuwa mkuu wa kitivo.
Mwaka 2023, Kithure alichaguliwa kuwa Seneta wa kaunti ya Tharaka Nithi na pia kuteuliwa kuwa kiongozi wa wengi.
Alichaguliwa Seneta kwa muhula wa pili katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2017 akichaguliwa pia kuwa naibu Spika,ila akatimuliwa mwaka 2020.
Kindiki ameteuliwa Waziri wa usalama wa kitaifa mwaka 2022 na Rais William Ruto, hadi alipoteuliwa tena kuwa Naibu Rais na kuidhinishwa na mabunge yote mawili, kufuatia kutimuliwa kwa Rigathi Gachagua.
Kindiki ana mke mmoja Joyce Gatiiria Njagi aliyemwoa mwaka 2001 na wamejaliwa na watoto watatu.
Profesa Kindiki atakuwa Naibu Rais wa 14 katika historia ya Kenya na wa tatu chini ya Katiba mpya iliyorasimishwa mwaka 2010.