Washukiwa wawili wa ujambazi wakamatwa Busia

Tom Mathinji
1 Min Read
Washukiwa wawili wa ujambazi wakamatwa Busia.

Maafisa wa idara ya upelelezi wa makosa  ya jinai (DCI),  wamewakamata washukiwa wawili wa ujambazi ambao wamekuwa wakiwahangaisha wakazi wa Busia.

Boniface Nyongesa Masakari na Denis Obelo Ekisa, walitiwa nguvuni katika maficho yao ya Malaba, baada ya maafisa hao wa polisi kupashwa habari za kijasusi.

Kupitia ukurasa wa X, DCI ilisema washukiwa hao walipatikana na bastola moja aina ya Tokarev iliyokuwa na risasi nane.

“Maafisa hao wa polisi walipata bastola aina ya Tokarev ikiwa na risasi nane katika nyumba ya Boniface Nyongesa,” ilisema DCI kwenye ukurasa wake wa X.

Wawili hao wanaaminika kuwa miongoni mwa kundi la majambazi wanaohusishwa na msururu wa wizi wa kimabavu katika mji wa Busia na viunga vyake.

Washukiwa hao wazuiliwa wakisubiri kufunguliwa mashtaka

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article