Wanawake Mandera waungana kushinikiza upatikanaji amani

Tom Mathinji
1 Min Read
Wanawake Mandera waungana kupigia debe upatikanaji wa amani na umoja.

Wanawake katika kaunti ya Mandera wameungana kwa lengo la kuhakikisha amani na umoja zinashuhudiwa katika kaunti hiyo ambayo imekumbwa na changamoto za kiusalama kwa muda mrefu.

Mchakato huo unaowaleta pamoja wanawake kutoka jamii tofauti, mashirika ya kijamii na wafanyabiashara, unanuia kupigia debe maelewano, mazungumzo na maridhiano miongoni mwa wakazi wa kaunti hiyo.

Likiongozwa na Nassin Dakane, kundi hilo linasisitiza kuwa ukuzaji wa amani hautafaulu ikiwa kila mmoja hatajumuishwa hasaa ushiriki wa wanawake.

“Amani haitapatikana bila kuwashirikisha wanawake  wa Mandera. Sisi ndio uti wa mgongo wa familia na jamii na sauti zetu zinapaswa kusikika katika kila mchakato wa kuleta amani,” alisema Dakane.

Wanawake hao walizindua mpango wa kuwafikia wanawake wenzao katika kaunti hiyo, ili kushirikiana nao katika kufanikisha juhudi za kuleta amani.

Aidha mchakato huo wa kuleta amani Mandera utajumuisha misururu ya mikutano itakayohusiha wadau mbali mbali, mikakati ya kuzuia mitafaruku na  kutekeleza mbinu bora za kupigia debe upatikanaji wa amabi.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article