Achani ahimiza Vijana wa Kwale kukumbatia mafunzo ya kiufundi

KBC Digital
1 Min Read
Gavana wa Kwale Fatuma Achani akimzawadi mwanafunzi aliyefuzu.

Gavana wa Kwale Fatuma Achani ameongoza hafla ya kufuzu kwa mahafala 60, pamoja na ugavi wa vifaa vya biashara ikiwemo vifaa vya ususi, pamoja na uzinduzi wa mpango wa Tujiajiri kwenye chuo cha mafunzo ya kiufundi cha Matuga huko mjini Kwale.

Akizungumza wakati wa hafla hio, Achani amewahimiza vijana kutoka Kaunti hio kuzingatia mafunzo ya vyuo vya kiufundi kama njia moja wapo yakujitengezea nafasi za kujiajiri, akisema serikali yake imekuwa mstari wa mbele kwa masuala ya vijana, ikiwemo ujenzi wa Vyuo 43 vya kiufundi pamoja na ruzuku ya shilingi milioni 30 itakayosaidia kufadhili masomo kwa vijana hasa wanaotoka kwenye familia zisizojiweza.

Kwa upande wake Mbunge wa Matuga Kassim Sawa Tandaza, amesema kuwa mpango wa Tujiajiri na Tandaza, unalenga kubuni nafasi nyingi za ajira kwa vijana wanaotoka katika eneobunge hilo, ili kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira miongoni mwao

Kulingana na Mgeni Mwamoyo, mmoja wa wanafunzi 60 waliohitimu katika chuo hicho ameshukuru juhudi za serikali ya kaunti ya Kwale na ile ya kitaifa kupitia kwa mfuko wa NG-CDF, akisema mafunzo pamoja na vifaa vya biashara walivyopata vitawasaidia kujibunia nafasi za ajira.

KBC Digital
+ posts
Share This Article