Washukiwa watatu kuendelea kuzuiliwa kwa madai ya mauaji ya mzazi wao

Regina na washukiwa wenzake,walikuwa wamewasilisha ombi la kuachiliwa ili waweze kuhudhuria mazishi yaliyopangwa kufanyika Jumanne wiki ijayo.

Tom Mathinji
1 Min Read
Mahakama ya Kibera.

Mahakama ya Kibera imeruhusu kuendelea kuzuiliwa kwa washukiwa watatu wanaodaiwa kumuua mzazi wao.

Watatu hao wanaojumuisha aliyekuwa mtangazaji wa runinga Regina Wambui Gitau almaarufu Regina Re, na wanafamilia wawili Thandie Malaika na Alton Jimmy Macharia, wanazuiliwa kufuatia kifo cha Dorita Lasinder Macharia mwenye umri wa miaka 86 nyumbani kwake katika eneo la Loresho jijini Nairobi, mnamo tarehe 30 Oktoba mwaka huu.

Regina na washukiwa wenzake,walikuwa wamewasilisha ombi la kuachiliwa ili waweze kuhudhuria mazishi yaliyopangwa kufanyika Jumanne wiki ijayo.

Hata hivyo, mahakama ilimwachilia mshukiwa wa pili, Emmanuel Munyeki ambaye anadaiwa kuwa mpenzi wa mjukuu wa marehemu baada ya upande wa mashtaka kusema  kuwa maelezo aliyotoa kwa polisi yaliungwa mkono na mashahidi wengine.

Wakili wa utetezi David Oyatta alipinga hatua ya kuzuiliwa kwao, akidokeza kuwa Thande malaika ni mwanafunzi na anatarajiwa kufanya mtihani.

Share This Article