Mtu mmoja amefariki na wengine watano kujeruhiwa, kwenye shambulizi la risasi siku ya Alhamisi Jijini Washington DC, nchini Marekani.
Kaimu Mkuu wa Polisi wa Washington DC Jeffery Carroll, amesema mshukiwa anayedaiwa kutekeleza shambuliza hilo alijifungia kwenye jengo moja, na polisi walipofika kwenye jengo hilo walimpata amefariki.
Kulingana na Carroll, maafisa wa polisi waliokuwa wakijadiliana na mshukiwa kwa njia ya simu walisikia mlio wa risasi, na baada ya hapo mshukiwa huyo alisitisha mawasiliano.
Polisi wamesema tukio hilo limetokea katika eneo la makutano ya barabara za 15th na P Street, kaskazini magharibi mwa jiji hilo, ndani na karibu na ukumbi wa mazoezi ya viungo saa mbili za asubuhi saa za nchi hiyo.
Hata hivyo, Maafisa wa Polisi wamesema bado hawajafahamu hali za watu watano waliopigwa risasi kwenye mkasa huo.