Mwanamume ahukumiwa miaka 20 gerezani kwa dhuluma za kimapenzi

Upande wa mashtaka uliwasilisha mahakamani cheti cha kuzaliwa cha mtoto huyo kuthibitisha umri wake ni miaka 13 uhalifu huo ulipotokea.

Tom Mathinji
1 Min Read
Mwanamume ahukumiwa miaka 20 gerezani kwa kumdhulumu mtoto kimapenzi.

Mahakama moja ya Nyeri, imemhukumu mwanamume miaka 20 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kumdhulumu kimapenzi mtoto mwenye umri wa miaka 13 katika eneo la Mukurwe-ini.

Mwanamume huyo alishtakiwa kuambatana na sehemu ya  8(1), pamoja na sehemu ya 8(3), ya sheria nambari tatu ya kukabiliana na uhalifu wa ngono ya 2006.

Mahakama ilifahamishwa kuwa mshtakiwa huyo alikuwa mfanyakazi wa shambani wa mjomba wa mtoto aliyedhulumiwa.

Kosa hilo liligunduliwa Agosti 14, 2025, wakati msichana huyo alitoweka mara kwa mara kutoka nyumbani kwao. Baadaye alipatikana nyumbani kwa mshtakiwa, na baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu, ilibainika alishiriki ngono na mshtakiwa huyo.

Upande wa mashtaka uliwasilisha mahakamani cheti cha kuzaliwa cha mtoto huyo kuthibitisha umri wake ni miaka 13 uhalifu huo ulipotokea.

Licha ya kuwa mshtakiwa huyo alikanusha kosa hilo, mahakama ilisema ushahidi wake haukutosha, huku ikipinga swala hilo litatuliwe kupitia maridhiano ya kifamilia.

Share This Article