Mkutano wa wajumbe wa vuguvugu la Linda Mwanchi (LLM) unaotarajiwa kufanyika leo Ijumaa Novemba 13, utaandaliwa faraghani .
Taarifa kutoka kwa kitengo cha masiliano cha muda cha LLM kikiongozwa Pauline Njoroge, IIisema kuwa wanahabari wala watu wasio wajumbe hawataruhusiwa kuingia.
Aidha,eneo la kuandaliwa kwa mkutano hao bado halijawekwa wazi na kuibua maswali mengi.
Mkutano huo unaotarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa muungano huo akiwemo Edwin Sifuna anayepigiwa upato kupokezwa bendera huenda ukaweka bayana maswala kadhaa ya uongozi kabla ya Sifuna kuanza ziara ya wiki mbili nchini Marekani kuanzia wiki ijayo kutafuta uungwaji mkono.