Amos Kipruto wa Kenya ameweka muda bora wa kibinafsi na kutwaa ubingwa wa makala ya 48 ya mbio za Chicago Marathon zilizoandaliwa Jumapili jioni nchini Marekani.
Kipruto ambaye aliwaacha wapinzani wake kwa umbali alikata utepe kwa muda wa saa 2 dakika 1 na sekunde 9.
Kipruto alimaliza wa tatu katika mbio hizo mwaka 2024 na kuchukua nafasi ya pili mwaka jana.
Tadese Bikila na Milkesa Mengesha wa Ethiopia walichukua nafasi za pili na tatu kwa saa 2 dakika 2 na sekunde 56, na saa 2 dakika 3 na sekunde 46 mtawalia.
Daniel Mateiko wa Kenya walichukua nafasi ya sita.
Bingwa wa Boston marathon mwaka huu Sharon Lokedi alimaliza wa pili akiwaongoza Wakenya kutwaa nafasi 2 hadi tano katika mbio za wanawake kwa kutumia saa 2 dakika 14 na sekunde 7 .
Bridgid Kosgei alichukua nafasi ya tatu ,akifuatwa Mary Ngugi Cooper na Joan Kilimo katika nafasi za nne na tano mtawalia.