Adel Amrouche ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Rwanda almaarufu Amavubi, kwa mkataba wa miaka miwili.
Shirikisho la soka nchini Rwanda (FERWAFA), lilimzindua Amrouche jana huku akiwa na kibarua cha kuifuzisha Amavubi kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika AFCON mwaka 2027.
Amrouche, ambaye zamani alikuwa kocha wa Taifa Stars ya Tanzania, atasaidiwa na Eric Nshimiyimana na Carolin Braun.
Kocha huyo amezinoa timu za Kenya, Libya, Burundi, Botswana, Yemen, na Tanzania huku ilihali upande wa vilabu amekuwa na USM Alger na MC Alger, zote za Algeria.