Washukiwa wa mauaji ya mbunge Charles Were kufikishwa mahakamani Jumatano

Tom Mathinji and KBC Digital
1 Min Read
Mbunge wa Kasipul Charles Ong’ondo Were.

Washukiwa watano wa mauaji ya mbunge wa Kasipul marehemu Charles Ong’ondo Were, watafikishwa mahakamani hii leo Jumatano.

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Renson Ingonga, siku ya Jumanne aliidhinisha mashtaka ya mauaji dhidi yao.

Washukiwa hao wanatarajiwa kufikishwa kwenye mahakama za Kibera na Milimani .

Washukiwa watatu William Imoli almaarufu kama Imo, Edwin Oduor Odhiambo almaarufu kama Machuani, na  Ebel Ochieng almaarufu kama Dave Calo watafikishwa katika mahakama kuu ya Kibera .

Washukiwa wengine Allan Omondi Ogola aliyekuwa mlinzi wa mbunge huyo pamoja na Isaac Kuria almaarufu kama Kush, ambaye uchunguzi unaonyesha ndiye aliyempiga risasi mbunge huyo watafikishwa kwenye mahakama kuu ya Milimani.

Uchunguzi unaonyesha kuwa watano hao pamoja na wengine walipanga na kumuua Ong’ondo Were Aprili 30,2025 mwendo wa saa moja na dakika 40 jioni.

Mauaji hayo yalitekelezwa karibu na chumba cha wafu cha City kwenye barabara ya Ngong, kaunti ndogo ya Kilimani hapa Nairobi .

Website |  + posts
Share This Article