Gladys Wairimu Kariuki, mke wa marehemu GG Kariuki, ameaga dunia.
Kulingana na msemaji wa familia Jimmy Waigwa, Bi. Kariuki alifariki alipokuwa alipokea matibabu katika hospitali moja Nairobi.
Gladys, aliyezaliwa mwaka 1945, anatambulika sana katika kaunti ya Laikipia kwa juhudi zake za kuimarisha jamii.
Mkulima huyo maarufu katika wadi ya Rumuruti, pia alikuwa kiongozi wa Maendeleo ya Wanawake tawi la Rumuruti, na alikuwa mwalimu katika shule ya msingi ya Ngarenaro, mjini Nyahurur.
Atakumbukwa sana kwa juhudi zake za kuwaunganisha na kuwaimarisha wanawake Kupitia miradi kadhaa ya maendeleo.
Gladys alikuwa mwanachama wa kanisa la Presbyterian Church of East Africa (PCEA), ambapo alihusika katika shughuli kadhaa za kanisa hilo Rumuruti, Nyahururu na Nairobi.
Amewaacha watoto watano, wajukuu na vitukuu.
Weledi wake utakumbukwa na wenvi daima.