Wanawake watatu mahakamani kwa kumkatili mwanamke

Dismas Otuke
1 Min Read

Wanawake watatu wamefikishwa katika mahakama ya mjini Eldoret kwa kosa la unyanyasaji wa kijinsia.

Kwa mujibu wa kesi hiyo, watatu hao – Monicah Jeptum, Joyce Jerobon na Caroline Jerotich walimwita mwanamke mwathiriwa chumbani mwa mmoja wa watatu hao ambapo walimjeruhi kwa mateso na hata kutia pilipili kwenye sehemu zake nyeti kwa madai kuwa mwanamke huyo yumo katika mapenzi na waume zao.

Kwa uchungu, alipiga ukemi mkali uliopelekea majirani kumunusuru na kumshauri aende hospitalini.

Baadaye, alipiga ripoti kwa kituo cha polisi cha Kapseret kisha watatu hao wakatiwa nguvuni.

Wakati wa kesi, shahidi mmoja alisema kuwa, “Tulisikia muhasiriwa akipiga mayowe kutoka chumbani mwa tukio na tulipoenda humo, tulimpata akiwaomba msamaha watuhumiwa. Tuliingilia kati na kumshauri aende hospitalini”. Alisema shahidi.

Washukiwa hao pia walishtakiwa kwa kosa la kumvamia na kumjeruhi mwathiriwa katika soko la Kapsaret mwezi wa Oktoba mosi.

Hata hivyo,walikanusha mashtaka na kuachiliwa kwa pesa taslimu ya shilingi 10,000 kila mmoja.

Kesi hiyo itasikilizwa tarehe 4/11/2024

TAGGED:
Share This Article