Gavana wa zamani wa Kiambu Ferdinand Waititu, mkewe Susan Wangari na afisa mmoja wa zamani wa kaunti hiyo, watafahamu hatima kuhusu kesi ya ufisadi inayowakabili juma lijalo.
Mahamaka imeagiza waendelee kuzuiliwa korokoroni hadi Jumanne Oktoba 27, 2026 wakati ambapo maelezo yatatolewa kuhusu ni nani atakayepunguziwa adhabu au kuhukumiwa baada ya mahakama kuu kuwapata na hatia katika kashfa ya ulanguzi wa pesa.
Hakimu mkuu Harrison Barasa aliahirisha kikao cha kusikizwa kwa suala hilo katika mahakama ya hakimu ya kukabiliana na ufisadi, baada ya upande wa mashtaka na ule wa utetezi kukosa kuafikiana kuhusu ikiwa washtakiwa hao wanapaswa kushtakiwa binafsi au kwa pamoja.
Haya yanajiri baada ya kesi hiyo kurejeshwa kwa mahakama ya hakimu ya kushughulikia kesi za ufisadi, kufuatia uamuzi wa mahakama kuu uliotolewa mnamo Oktoba 14 mwaka huu.
Uamuzi huo ulibatilisha uamuzi wa kutowapata na hatia kuhusiana na mashtaka ya ulanguzi wa pesa na kuwapata na hatia kwenye kesi ya ufisadi iliyohusisha shilingi milioni-588.
Hakimu huyo amesema atafuta ushauri kutoka kwa mahakama kuu, kabla ya kuendelea na mchakato wa kutoa hukumu.