Wahudumu wa afya wa UHC waandamana Turkana

KBC Digital News
1 Min Read
Picha ya awali

Wahudumu 150 wa afya chini ya mpango wa afya kwa wote (UHC) waliopaswa kuajiriwa kwa mktaba wa kudumu, wameandamana kulalamikia kucheleweshwa kuajiriwa na serikali ya kaunti ya Turkana. 

Wanaituhumu serikali hiyo kwa kuwapuuza.

Kwa mujibu wa wahudumu hao, hawajapokea barua za kuthibitishwa kuajiriwa wala kupokea mshahara wa miezi mitatu licha ya kuripoti kazini.

Wanadai Bodi ya Utumishi wa Umma ya kaunti hiyo imewafumbia macho.

Licha ya serikali kuu kutenga fedha kupitia mgao wa ziada wa serikali za kaunti (CGAA) kwa ajili ya kuwaajiri, wanasema Bodi ya Utumishi wa Umma ya kaunti ya Turkana imewaeleza kuwa haijapokea fedha hizo.

Share This Article