Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia wakimbizi wa Palestina United Nations Relief and Works Agency for Palestine Refugees – UNRWA wamefutwa kazi.
Israel ilitoa taarifa ambazo zilihusisha wafanyakazi wapatao 12 wa UNRWA na mashambulizi ya wapiganaji wa Hamas katika maeneo mbali mbali ya Israel Oktoba 7, 2023.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa taarifa kuhusu suala hilo akisema kwamba shirika hilo linachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi hao.
Kulingana naye uchunguzi ulianzishwa mara moja na wafanyakazi hao 12 wakatambuliwa. Guterres anasema 9 kati yao walifutwa kazi na Kamishna Mkuu wa UNRWA Philippe Lazzarini.
Mmoja amethibitishwa kufariki na utambuzi wa wengine wawili bado haujatekelezwa.
Guterres ametoa onyo kali kwa wafanyakazi wote wa Umoja wa Mataifa akisema yeyote atakayepatikana na hatia ya kuhusika kwenye ugaidi atachukuliwa hatua.
Katibu huyo mkuu anasema watu milioni 2 katika ukanda wa Gaza wanategemea misaada ya shirika la UNRWA lakini ufadhili wa sasa hautoshi kutekeleza jukumu hilo mwezi ujao.
Kutokana na madai ya wafanyakazi wa UNRWA kuhusika kwenye mashambulizi yaliyosababisha vita vinavyoendelea katika ukanda wa Gaza, baadhi ya wafadhili wakuu wa shirika hilo wamejiondoa.
Marekani kupitia wizara yake ya mambo ya nje imetangaza kusitishwa kwa ufadhili zaidi kwa UNRWA hadi madai hayo yashughulikiwe.
Msemaji wa wizara hiyo Matthew Miller alisema kwenye taarifa kwamba madai ya wafanyakazi wa UNRWA kuhusika kwenye mashambulizi ya Israel ni ya kuhuzunisha.
Philippe Lazzarini hata hivyo ameomba nchi ambazo zimekuwa zikifadhili UNRWA kutafakari upya kuhusu hatua ya kusimamisha ufadhili.