Wanaochangia mradi wa nyumba kupokea mkopo kwa riba ya chini

Ruto amesema watapitisha  sheria bungeni kuwawezesha wote wanaochangia mradi huo  kupokea mkopo wa shilingi milioni 5 kwa riba chini ya asilimia 10.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto ametangaza kuwa Wakenya wote wanaotozwa ushuru wa nyumba wataanza kupokea mkopo kwa riba ya chini ya silimia 10 ili kununua na kumiliki nyumba hizo.

Ruto amesema watapitisha  sheria bungeni kuwawezesha wote wanaochangia mradi huo  kupokea mkopo wa shilingi milioni 5 kwa riba chini ya asilimia 10.

Alisema kuwa hatua hiyo itawawezesha Wakenya kuwa na fursa ya kumiliki nyumba hizo.

Aidha,Ruto aliusifia mradi huo wa nyumba za gharama nafuu akisema kuwa umebuni nafasi za ajira  zaidi ya laki mbili unusu na kubadili maisha ya wengi.

Rais amesema haya kwenye hotuba yake ya maadhimisho ya 62 ya sherehe za siku kuu ya Madaraka katika uwanja wa Raila Odinga kaunti ya Homabay.

Website |  + posts
Share This Article