Waalikwa Red Arrows watwaa kombe la CECAFA

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa wa Ligi Kuu nchini Zambia Red Arrows ndio washindi wa mwaka huu  wa kombe la muungano wa vyama vya soka Afrika mashariki na kati CECAFA.

Fainali hiyo ilisakatwa katika uchanjaa wa KMC jijini Dares Salaam.

Arrows  ambao wamekuwa wakishiriki mashindano hayo kama waalikwa wametwaa ubingwa Jumapili jioni jijini Dares Salaam Tanzania,baada ya kuwashinda Rwanda Partiotic Army (APR) penati 10-9 kufuatia sare ya bao 1-1.

Ricky Banda akiwaweka Arrows uongozini kunako dakika ya 62,lakink iliwabidi APR, wasubiri hadi dakika ya 91 wakati Mamadou SY alipokomboa goli hilo.

Ni mara ya kwanza  kwa Arrows kushinda kombe la CECAFA,  baada ya timu kuu kama vile Yanga na Simba na pia wapinzani wa Uganda kususa.

Al Hilal kutoka Sudan walimaliza nafasi ya tatu baada ya kuwalemea Al Waday, mabao 3-2 kupitia mikiki ya penati baada ya dare ya bao 1.

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *