St. Antony na JOBO kuchuana tena

Boniface Mutotsi
2 Min Read

Kamati ya kutatua mizozo baina ya shule za upili ya kaunti ya Trans Nzoia imeamuru mechi iliyotibuka baina miamba wa soka nchini – St. Antony (KD) na St. Joseph ( JOBO ) kurejelewa.

Uamuzi huo unafuatia kesi iliyowasilishwa na JOBO kuwa KD ilitumia wachezaji wawili waliozidi miaka 19 inayohitajika.

Kwa mujibu wa duru za kuaminika, kamati hiyo ilifanya uchunguzi ila haikuwapata wawili hao na hatia hivyo ikaamuru mechi hiyo kurudiwa.

Katika mechi ya nusu fainali ya kaunti iliyotibuka ugani Ndura mjini Kitale, KD ilikuwa uongozini wa mabao matatu kwa mawili.

Namo dakika ya 81, JOBO ilisusia kucheza kwa madai ya kunyimwa tuta.

Baadaye, iliwasilisha kesi ambayo uamuzi wake umeibua maswali mengi miongoni mwa wafuasi wa timu hizo na wapenzi wa soka kwa jumla.

Kamati hiyo vile vile imeamuru ngarambe zingine zenye utata – Bwake dhidi ya Goseta na vipusa wa Wiyeta dhidi ya wale wa St. Joseph kucheza upya.

Uamuzi mwengine unaosubiriwa kwa hamu na ghamu juma hili ni baina ya shule ya wavulana Kakamega ( Green commandoes) na Musingu ( The scorpions) za Kaunti ya Kakamega.

Kule, madai ni sawia na yale ya JOBO ambapo Kakamega wanawatuhumu Musingu kwa kutumia wanafunzi kadhaa waliozidi umri nao Musingu wanajibu Kwa wanadai kwamba kakamega walitumia majina ghushi ya mwafunzi mmoja.

Kesi hiyo inajiri baada ya Musingu kuipiku Kakamega kwa matuta ya 5 -4 kwenye nusu fainali ya michezo baina ya shule za upili za kaunti hiyo.

Boniface Mutotsi
+ posts
Share This Article