Mataifa 13 yamefuzu kwa makala ya 23 ya kipute cha Kombe la Dunia mwaka ujao katika mataifa ya Mexico,Marekani na Canada.
Timu zilizofuzu ni pamoja na sita ya bara Asia: Australia, Iran, Japan, Jordan, Korea Kusini, na Uzbekistan; matatu ya eneo la CONCACAF wakiwa wenyeji watatu: Canada, Mexico, na Marekani; matatu ya eneo la CONMEBOL: Argentina, Brazil, Ecuador, na New Zealand kutoka eneo la Oceania.
Jumla ya mataifa 48 yatashiriki fainali za Kombe la Dunia za mwaka ujao kwa mara ya kwanza, ikiwa ongezeko kutoka idadi ya timu 32.