Vipusa wa Kenya,KCB na Pipeline kucheza nusu fainali dhidi ya wenyeji Ijumaa usiku

Dismas Otuke
1 Min Read
Waakilishi wa Kenya katika  mashindano ya kilabu bingwa Afrika ya Voliboli ya vipusa Kenya Commercial Bank-KCB, na Kenya Pipeline-KPC, watashuka uwanjani Ijumaa kwa nusu fainali dhidi ya timu za Misri ambao wanaandaa mashindano hayo.
KPC  ya Kenya itakuwa ya kwanza kushuka dimbani jijini Cairo dhidi ya Al Ahly kuanzia saa moja usiku majira ya Afrika mashariki kabla ya KCB kukabana koo na Zamalek saa tatu usiku.
KPC walitinga fainali Jumatano baada ya kuwazabua Lito Team ya Cameroon seti tatu kwa bila za 25-22,25-20 na 25-15 katika roboro fainali.
KCB nao walijikatia tiketi kwa semi fainali baada ya kuwatema wenzao Kenya Prisons seti tatu kwa sufuri za 25-20,25,22 na 25-17 katika kwota fainali.
Ili kufuzu kwa nusu fainali Zamalek waliibwaga Mayo Kano Evolution ya Cameroon seti tatu bilajibu za 25-13,25-17,26-24.
Ahly walitinga awamu ya nne bora baada ya kuwachachafya National Alcohol and Liquor Factory ya Ethiopia kwa seti za 25-10,25-11 na 25-10.
TAGGED:
Share This Article