Mercy Kwambai na Samson Lemayan ndio mabingwa wa makala ya 25 ,ya mbio za kila mwaka za Lewa Safari Marathon, zilizoandaliwa Jumamosi katika hifadhi ya wanyamapori ya Lewa kaunti ya Meru.
Kwambai aaliye na umri wa miaka 36 alizitiumka mbio hizo kwa muda wa saa 2 dakika 47 na sekunde 17,akifuatwa katika nafasi ya pili na Evaline Lagat kwa muda wa saa 3:02:31 na Monica Watetu aliyemaliza wa tatu kwa saa 3:02:31 and 3:20:21 .
Samson Lemayan wa Maralal alitawazwa bingwa wa mbio za wanaume akiziparakasa kwa saa 2 dakika 28 na sekunde 35 ,akifuatwa na John Musee kwa saa 2 dakika 29 na sekunde 31 huku Joseph Kariuki, akiambulia nafasi ya tatu ,sekunde 6 baadaye.
Michael Kamau alitumia muda wa saa 1 dakika 6 na sekunde 37, kushinda mbio za nusu marathon,akifuatwa na Justine Lelitan na Simon Saidimu katika nafasi za pili na tatu mtawalia.
Mary Waithera, alishinda mbio za kilomita 21 wanawake kwa saa 1 dakika 18 na sekunde 27,akifuatwa na Pauline Ngigi na Susan Wanjiru, waliomaliza nafasi za pili na tatu kwa saa 1 dakika 28 na sekunde 21 na saa 1 dakika 29 na sekunde 4.
Washindi kilomita 42 na nusu marathon walituzwa shilingi laki moja unusu huku waliomaliza nafasi za pili wakiondoka na shilingi 80,000, huku waliochukua nafasi za tatu wakiondoka na shilingi 60,000.