Viongozi kadhaa wa Afrika wanahudhuria uzinduzi wa ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote kaunti ya Lamu.
Miongoni mwa wale waliohudhuria hafla hiyo ya kihistoria ni Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, mwenzake ya Benin Wadagni Romuald na Jean-Lucien Sayi de Tove wa Togo.
Wengine ni Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na Rais mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo.
Sherehe ya uzinduzi wa ujenzi huo inaongozwa na Rais William Ruto na mwekezaji bilionea wa Nigeria Aliko Dangote.
Ujenzi wa kiwanda hicho unatarajiwa kugharimu kitita cha shilingi trilioni mbili, na baada ya kukamilika, kitazalisha mapipa 700,000 ya mafuta pamoja na kutoa nafasi za ajira 60,000 kwa vijana wa eneo hilo.
Mradi huo unatarajiwa kuchukua muda wa miaka mitatu kukamilishwa na utatoa bidhaa zilizosafishwa za mafuta kwa Kenya na mataifa jirani.