Ushirikiano kati ya serikali kuu na kaunti ya Nairobi: Kamati yakutana

Martin Mwanje
1 Min Read
Kamati ya kuratibu ushirikiano kati ya serikali kuu na serikali ya kaunti ya Nairobi

Kamati ya Pamoja juu ya Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Serikali Kuu na Kaunti ya Nairobi ilikutana leo Ijumaa kutafuta mbinu za kuboresha utoaji huduma katika kaunti hiyo. 

Kamati hiyo inaongozwa na Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi na wanachama wengine wanajumuisha Mawaziri Opiyo Wandayi wa Nishati, Dkt. Deborah Barasa wa Mazingira na Kipchumba Murkomen wa Usalama wa Taifa.

Mwanasheria Mkuu Dorcas Oduor pia ni mwanachama.

“Kama Mwenyekiti wa Kamati Simamizi, tuliangazia mapitio ya mikakati ya uwajibikaji, mipango ya kupewa kipaumbele na makataa ya utimizaji wa mipango hiyo ili kuhakikisha Makubaliano hayo yanaboresha usambazaji maji, usafi, uwekaji taa, uboreshaji barabara na usalama wa mji,” alisema Mudavadi baada ya mkutano huo.

Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja ametetea vikali makubaliano kati ya serikali kuu na serikali ya kaunti akisema yatasaidia kuboresha huduma zinazotolewa kwa wakazi.

Amekanusha madai ya kuhamishia majukumu ya kaunti kwa serikali kuu.

 

Share This Article