Uongozi wa EAC wafanyiwa mabadiliko

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameteuliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Jumuiya hiyo

Martin Mwanje
1 Min Read
Rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC imepata uongozi mpya.

Hii ni baada ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni kuteuliwa kuwa mwenyekiti mpya wa jumuiya hiyo.

Museveni anachukua mahali pa Rais William Ruto ambaye ameondoka baada ya kuhudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Rais Ruto aliteuliwa kwenye wadhifa huo Novemba 30 mwaka 2024.

Uenyekiti wa jumuiya hiyo ni wa kubadilishana zamu kati ya Marais wa nchi wanachama kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Wakati huo huo, Balozi Stephen Patrick Mbundi kutoka Tanzania ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa EAC.

Anachukua mahali pia Veronica Nduva anayeondoka baada ya kuhudumu kwa kipindi cha zaidi ya miezi 20.

Nduva aliteuliwa kama Katibu Mkuu wa EAC Juni 7 mwaka 2024.

Share This Article