Zaidi ya watoto milioni nane hawaendi shuleni kutokana na vita nchini Sudan, Umoja wa Mataifa umesema.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed, alitoa onyo hilo siku ya Ijumaa wakati wa mkutano usio wa kawaida kuhusu kulinda elimu nchini Sudan, huku vita vya wenyewe kwa wenyewe vikiingia siku ya a 1,210.
“Miongoni mwa maswala ambayo vita hivi ninahujumu, ni mustakabali wa Sudan, kuwanyima watoto wake elimu,” alisema Mohammed akidokeza kuwa ghasia hizo na kunyima kizazi kipya mustakabali.
Kulingana na Umoja wa Mataifa, takribani robo tatu ya shule zote nchini Sudan zimeharibiwa au haziwezi tumika, tangu mapigano yalipozuka Aprili 2023.
“Watoto watano kati ya sita hawaendi shuleni, na wazazi watakueleza kuwa afadhali watoto wasalie nyumbani badala ya kwenda shuleni, kwa sababu nyumbani ndio mahala tu salama,” aliongeza Mohammed.
Aidha, kulingana na Mohammed, nusu ya walimu nchini Sudan hawapokei mishahara, ingawa wengine wanaendelea kufanya kazi.